Tanzania

Rais Mwinyi Awakaribisha Wafanyabiashara Wa Uingereza Kuwekeza Zanzibar

APRILI 8, 2025
Border
news image

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka Uingereza kuwekeza Zanzibar katika fursa mbalimbali ikiwemo sekta ya uchumi wa buluu, utalii, usafiri wa baharini, uvuvi, nishati na miundombinu ya kidijitali.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipojumuika kwenye chakula cha jioni na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za biashara na uchumi za Uingereza kilichoandaliwa na Taasisi ya Eastern Africa Association ya Uingereza katika Jiji la London Aprili 2025.

AM/MTV News DRC