DRC

Usafiri Pamoja Na Kazi Zengine Zimesimamishwa Siku Ya Juma Tano Hii 09 April 2025 Katika Mji Wa Manguredjipa Secta La Bapere Wilayani Lubero Kivu Kaskazini Baada Ya Muendesha Pikipiki Wa Shirika ATAMOV Kuuwawa N'a Kuzikwa Na Watu Wenye Kumiliki Silaha

APRILI 9, 2025
Border
news image

Vikundi vya waendesha pikipiki vimetangaza mugomo hii juma ine baada ya kuelekea mahali alipozikwa baada ya kufariki kwa kupigwa fimbo, Mumbere Chevo de Gauche, mzaliwa wa Vuyinga mwenye umri wa miaka 24, kwenye eneo la Fatua karibu kilometa 12 kaskazini-mangaribi mwa Manguredjipa. Wakishutumu hali hiyo ya unyanyasaji dhidi ya raia, waendesha pikipiki walitangaza mugomo usiokoma kwa waendesha pikipiki hadi viongozi kupata suluhuhisho kwa la haraka.

Kazi za usafiri pia za kibiashara zilisimamishwa juma tano hii ikiwa siku ya kwanza ya mugomo.

Esdras Kamathe, ni naibu kiongozi wa shirika ATAMOV Manguredjipa, aomba kuondoa watu hao wenye silaha eneo hilo kwa haraka.

Kagheni Samuel, kiongozi wa mashirika ya shirika la kiraia katika secta la Bapere, ashutumu mauaji ya mwendesha pikipiki inayo tokea mara kwa mara kwa sasa kukiwa hakuna suluhisho. Samuel ameomba wapiganaji wazalendo kuondoka eneo hilo kwani wameyumbisha sasa usalama wa wananchi.

Wakati huo huo, vijana wa kabila la Wapiri washutumu mugomo wa wafanyakazi wa secta la Bapere ulioanzishwa tangu juma tatu iliyo pita wakishutumu uongozi usio jibu mahitaji ya wakaazi ya viongozi wa secta la Bapere. Katika matamshi yake, Régis Kanzuli kiongozi, aomba viongozi kuwajibika kwa ajili ya kukuza uchumi wa eneo husika.

AM/MTV News DRC