Vituo vya afya vilivyo fungua milango yake tangu January elfu mbili ishirini na tano vya shindwa kujibu mahitaji ya wanajeshi pia raia kutokana na upungufu wa dawa. Baadhi ya wafanya kazi wa afya wasema hali ni mbaya na wameshindwa kujimudu kimaisha kutokana na hali ambayo ni ngumu ya bila mapato, wagonjwa wakishindwa kulipa dawa baada ya kupata tiba kutokana na ukosefu wa pesa kwani shamba zao hazina usalama.
Paluku Nzanzu Achile, muratibu wa shirika la kiraia katika eneo la Manzia, aomba serikali kusaidia wakaazi na wananchi wa Congo DRC hasa wanaopatikana eneo la Mangurudjipa ambao wameathirika kwa muda mrefu na mashambulizi ya watu wanaodhaniwa kuwa ADF, ambao wamesha lazimisha wakaazi kuhama mashamba na makaazi yao kutokana na ukosefu wa usalama. Wengi wakishambuliwa na kuuawa wanapojaribu kuelekea mashambani.
Upande wa mkuu wa wilaya ya Lubero, Bwana Mitela Kiwewa Alain, ni muhimu kwa wafanya kazi walioanza mgomo wa kazi kuendelea kusaidia wakaazi ambao bado hawana uwezo wowote wa kujikimu kimaisha. Wachambuzi wakishutumu serikali kwa kushindwa kuelewa matatizo wanayopitia wafanya kazi wa afya pamoja na wale wa serikali katika maeneo ambazo kwa sasa zinakabiliwa na ukosefu wa usalama, kama Mangurudjipa, ambako hali ya kimaisha kwa sasa ni ngumu.